Makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akitibitisha kumufukuza kazi kocha mbelgiji Thom Saintfiet. |
Timu Ya Dar es salaam Young African leo imetoa taarifa rasmi ya kusitisha kandarasi na mkufunzi mkuu wa
timu hiyo ,raia wa ubelgiji Tom Saintfiet
huku nafasi yake ikikasimiwa na aliyekuwa msaidizi wake , Freddy Felix Minziro mpaka atakapo patikana
mkufunzi mpya wa timu hiyo Makamu
Mwenyekiti wa vaa ndala hao za kijani na manjano , Clement Sanga amesema kuwa , matokeo yasiyoridhisha ndio yaliyosabisha menejiment isitishe
kandarasi ya Saintfiet.
Hatimaye
uongozi wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Yanga, umethibitisha kumuondoa kazi kocha mkuu
wa klabu Thom Saintfiet kwa kukatisha mkataba wake kwa kile kilichoolezwa kuwa
ni kwenda kinyume na maagizo ya mwajiri wake.
Akiongea na
waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe hapa nchini Clement
Sanga, amesema uongozi wa Yanga haukuridhishwa na hatua ya kocha huyo
kuirejesha timu Dar es Salaam mara baada ya mchezo wao wa kwanza uliofanyika
mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons.
Jana usiku
kiliitishwa kikao cha viongozi wa juu wa Yanga na kocha Thom, kujadiliana juu ya mwenendo mbaya
wa kimatokeo wa timu hiyo ambayo mpaka sasa Yanga ina point moja baada ya
kushuka dimbani mara mbili.
Mkurugenzi mpya wa fedha Yanga Denis Oundo |
Kikao hicho
kilikumbwa na mzozo kufuatia kocha Thom kuonyesha msimamo wake kwa yale anayo
yataka pamoja na kujitetea kufuatia matokeo mabaya ya kwenda sare ya bila
kufungana na Prisons na kufungwa mabao 3-0 na Mtibwa.
Kilicho pelekea
maamuzi hayo magumu ni suala la kubwatukiana na mwenyekiti wake Yusufu Manji ambaye
naye kwa mamlaka yake aliamua kumfukuza katika kikao na uongozi kuendelea na
kikao chao ambacho kilitoka na maamuzi ya kumkatisha mkataba wake.
Taarifa zinasema kocha
huyo alilazimisha kurejea Dar es Salaam wakati kwa kujibu wa program ya klabu
ni kuwa alipaswa kuipeleka timu mkoani Morogoro siku mbili kabla ya mchezo wao
dhidi ya Mtibwa kujiandaa na mchezo huo jambo ambalo lingepunguza uchovu kwa
wachezaji ambao unatokana na safari.
Fredy Minziro |
Sababu nyingine
ambayo imetolewa na Sanga ni kuwa kocha huyo aliwaruhusu wachezaji kutoka usiku
kwenda kwenye majumba ya starehe baada ya kumaliza mchezo wao dhidi Tanzania
Prisons, jambo ambalo amesema ni kwenda kinyume na taratibu za kambi na pengine kuendelea kusababisha matokeo mabaya kwa Yanga.
Sanga
amesema kitendo cha kukaidi agizo hilo ni kwenda kinyume na maagizo ya uongozi
ambao ndio mwajiri wake.
Sababu nyingine
ni kuwa kocha huyo alikuwa akitaka timu isikae kambini isipokuwa wachezaji wawe
wanakusanyika siku tatu kabla ya mchezo.
Clement
Sanga amemtangaza Fred Felix Minziro aliyekuwa kocha msaidizi sasa
kukaimu nafasi ya Thom Saintrfiet kuanzia hii leo mapaka hapo atakapo
patikana kocha mwingine.
Katika
hatua nyingine makamu mwenyekiti huyo wa Yanga amemtaja Laurence
Mwalusako kuwa kaimu katibu mtendaji wa Yanga katika kipindi hiki na
pia amemtangaza Denis Oundo kuwa mkurugenzi wa fedha.
No comments:
Post a Comment