HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 October 2012

(ECAPBA) YATOA KIBALI

Chama Cha ngumi za Kulipwa cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimetoa kibali kwa promota Selemani Seminyo cha kuandaa pambano la kugombea ubingwa wa wa Afrika ya mashariki na Kati katika uzito wa kati (middleweight) baina ya bondia Thomas Mashali wa Tanzania na Sebayala Med wa Uganda.
Pambano hilo litafanyika katika ukukumbi wa Friends Corner, Manzese, jijini Dar-Es-Salaam, siku ya Jumapili tarehe 14 October, 2012.
ECAPBA inajivunia kuwawezesha mabondia wengi kutoka katika nchi wanachama kuendeleza vipaji vyao kwa kugombea mikanda ya ubingwa wake.
Tanzania ina bahati ya kufanya mapambano mengi ya ubingwa wa ECAPBA na tunao mabondia wengi ambao ni mabingwa ikilinganishwa na nchi nyingine.
Nchi wanachana wa ECAPBA ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Ethiopia, Sundan ya Kusini, DRC Congo na Zambia.
ECAPBA ilipendekezwa kuundwa mwaka 2004 baada ya kikao cha kwanza nchini Kampala Uganda katika hoteli ya Ghana kikiwashirikisha viongozi toka Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia na Malawi na kufuatiwa na kikao cha uanzilishi mwaka 2004 katika hoteli ya Kilimanjaro Crane mjini Moshi, Tanzania.
ECAPBA inawaalika mapromota wengi kuandaa mapambano ya ubingwa kwa mabondia wengi kwani hii ji njia mojawapo ya kuinua viwango vya mabondai wetu.
Aidha, ECAPBA inawaomba wadau wa ngumi ikiwa ni pamoja na watu binafsi, makampuni, taasisi za serikali na binafsi zijitokeze kwa wingi kudhamini mapambano yake ya ubingwa kama njia mojawapo ya kuinua biashara zao na kuendeleza vipaji vya mabondia nchini!
Shirikisho la Ngumi la Afrika ya Mashariki na Kati limesajiliwa nchini Tanzania ambako ndipo palipo na makao yake makuu kwa sasa.
Viongozi wakuu wa ECAPBA ni:
Rais: Onesmo Alfred McBride Ngowi, TANZANIA
Makamu wa Kwanza wa Rais: Celestino Mindra, UGANDA
Makamu wa Pili wa Rais: George Uthman, KENYA
Katibu Mkuu: Shaaban Ogolla, KENYA,
Mweka Hazina: Nemes Kavishe, TANZANIA
Afisa Uhusiano: Paul Chiwa, UGANDA

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers