Mkenya, Victor Wanyama amefunga mabao mawili kwa
kuisadia klabu yake ya Celtic kuinyeshea klabu ya St. Mirren kwa mabao
5-0, na kuendeleza uongozi wao katika ligi kuu ya premier nchini
Scotland.
Ushindi huo umeipa Celtic matumaini makubwa huku
ikijiandaa kwa michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya
dhidi ya Barcelona.
Hata
hivyo, St Mirren ilipoteza nafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi
hiyo. Garry Hooper aliifungia celtic bao lake la kwanza kunako dakika ya
kumi na tano kabla ya Efe Ambrose kufungwa bao la pili.
Wanyama naye akafunga bao la tatu kunako dakika ya 32 na dakika chache baadaye Wanyama aklafunga bao la pili.
Kocha wa St Mirren Danny Lennon amesema
amehuzunishwa sana na matokeo ya mechi hiyo, kwani wachezaji wake
hawakucheza kama kawaida yao.
Lakini kocha wa Celtic, Neil Lennon amesema
mechi hiyo imekuwa fursa nzuri kwa wachezaji wake kujiandaa kwa mechi
yao ya wiki ijayo dhidi ya Barcelona
No comments:
Post a Comment