HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 October 2012

LIGI YA MISRI BADO KITENDAWILI


Chama cha soka cha mpira wa miguu cha misri kimeamua kuchelewesha baadhi ya mechi za ligi kuu ya nchi hiyo huku sababu kubwa ikiwa  hawajapewa taarifa za uhakika kuhusu kuwepo kwa usalama wa kutosha na serikali  mara baada ya kutoa machafuko katika bandari ya  Said miezi nane iliyopita .

Jumla ya watu sabini na nne  ambao wengi wao ni mashabiki wa timu yenye maskani yake katika jiji  Cairo club al-Ahly, klabu yenye mafanikio zaidi katika bara la afrika  ,Ambapo mashabiki hao waliuawa baada ya mashabiki wa  Port Said- ambaohushangilia timu yao ya  al-Masry kufanya vurugu  mwishoni mwa mchezo huo  
''Tumemuuliza waziri wa mambo ya ndani kuhusu swala la ulinzi lakini atujapata jibu lolote mpaka sasa katika taarifa iliyotolewa tovuti ya chama cha soka cha misri ."

Ligi hiyo ya Misri ilitakiwa kuendelea kutimua vumbi kuanzia kesho  October 17, lakini baadhi ya mashabiki wa  Ahly's wanaofahamika kama  ultras,   wametaka ligi hiyo iliendelee kusitishwa hadi pale watuhumiwa watakapo perekwa mbele ya mahakama kujibu tuhuma hizo  ambapo jumla ya washitakiwa 73 wanatuhumuiwa kuendesha mauaji hayo .
Tangu tukio hilo litokee kaskazini mwa jiji la port said February  Mosi mwaka huu , shughuri zote za soka zimesimamishwa ambapo katika historia ya misri haijawahi kutokea 

lakini taarifa kutoka katika maofisa wa shirikisho la soka la misri waliimbia tovuti ya Ahram  kuwa sababu kubwa ya kuchelewesha ni kuwa kamati mpya iliyochaguliwa inataka kusubiri hadi pale kesi itakapomalizika ili kuzipa familia zilizopoteza wapendwa wao kupata faraja  ambapo jumla ya maofisa tisa wa polisi na baadhi ya maofisa wa timu ya  Masry ni moja kati ya watuhumiwa   73 ambao wanahusihwa na machafuko hayo  aidha washitakiwa wengine wanakabiriwa na kesi ya mauaji wakati , Baadhi ya maofisa wanakabiriwa na tuhuma za kuasadia baadhi ya mashabiki kufanya fujo hizo. 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers