Sura
ya nje ya uwanja ya kumbukumbu ya CCM sokoine jijini Mbeya ambao ni uwanja wa nyumbani wa
Timu ya Prison inayoshiriki ligi kuu ukimilikiwa na Chama cha Mapinduzi
umekuwa miongoni mwa miradi iliyotelekezwa katika ujenzi wa miundo
mbinu yake hasa eneo la vyoo.
|
Hii
ni sehemu ya ndani ya uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambao umaarufu
wake unajulikana tangu miaka ya themanini ambapo Tukuyu starz ilipandia
daraja na kushiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza mwaka 1986 na kutwaa
ubingwa mwaka huo huo, lakini kadiri miaka inavyoenda mbele huduma za
uwanja zimekuwa zikirejea nyuma badala ya kuboreshwa |
|
Hiki
ni miongoni mwa vyoo vinavyotumiwa na mashabiki wanaolipa kiingilio cha
shilingi 3000 kwa mechi moja kwenye uwanja wa sokoine! Chama cha soka
mkoa kinalalamika kuwa mahudhulio ya mashabiki ni kidogo hivi sasa
katika uwanja huo, lakini kwa huduma hizi nani angependa kulipia huduma
yenye viwango hivi? |
|
Hapa
ndipo watumiaji walipofikia na kuendelea kupanga mizigo yao kuelekea
nje baada ya choo kutokuwa na huduma zozote za usafi ! Idara ya afya ya
halmashauri ya jiji imekuwa miongoni mwa taasisi za umma zinazolaumiwa
na wadau wa soka kwa kufumbia macho hali hii |
|
Hiki
ni moja ya vyoo vya pasport size kwenye uwanja wa sokoine ambavyo
vinatumika kwenye michezo ya ligi kuu na shughuli mbalimbali za ujio wa
viongozi kitaifa, uchaguzi mkuu wa chama na mikutano pamoja na matamasha
mbalimbali! |
|
Kamera
yetu imenasa mteja wa huduma za majengo haya zikiwa hazitosherezi na
hasa milango yake ambayo upana wake haumwezeshi mtu kuingia kwa urahisi
na badala yake kuingia kiubavu ubavu na matokeo yake watumiaji kuishia
mlangoni na kumaliza shida zao |
|
Haya
ndiyo mabafu ya uwanja wa sokoine jijini mbeya ambayo kwa sasa
yamekuwa yakitumika kama vyoo na baadhi ya watumiaji kutokana na hali ya
vyoo kuwa mbaya |
|
Ukuta wa duka la mojawapo lililo nje ya uwanja wa sokoine ukiwa unanyunyizwa kwa haja ndogo za watumiaji wake .
|
Hali
ya uwanja wa sokoine jijini Mbeya imeelezwa kuwa mbaya na huenda ikawa
chanzo cha magonjwa ya mlipuko katika jiji hilo wakati huu tukielekea
kwenye msimu wa masika
No comments:
Post a Comment