HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

3 October 2012

TANZANIA YAANGUKA FIFA, URENO YAINGIA TATU BORA UBORA WA FIFA DUNIANI



 Shirkisho la soka la dunia FIFA limetoa viwango vipya vya ubora ambavyo ni vya  mwezi uliopita  vinavyojulikana kama  FIFA/Coca cola baada ya kuchezwa kwa mechi mia moja thelathini na sita ambapo katika mechi hizo sabini na sita zilikuwa za kufuzu kwa fainali za kombe la dunia Mwaka 2014 huko Brazil.  


Ambapo timu zinazoshika nafasi ya juu kwa sasa ni  Spain na  Germany zimejikuta zikichuana huku Ureno ikishika nafasi ya Tatu na   Argentina ikishika nafasi ya nne wakati Colombia wao wakishika nafasi ya tisa ambao wameingia kwa mara ya kwanza katika kumi bora tangu mwaka 2002  walipoifunga chile mabao matatu kwa moja

Lakini kwa upande mwingine Tanzania imeporomoka katika viwango hivyo kwa nafasi moja baada na kukamata nafasi  ya mia moja ishinrini na nane huku Lebanon ikichukua nafasi ya Tanzania katika viwango hivyo vya fifa ambapo uganda bado inaongoza kwa afrika mashariki ikifuatiwa na kenya katika nafasi ya 126  wakati burundi yenyewe inashika nafasi ya mia moja thelathini na tatu viwango hivi hutolewa kila baada ya mwezi mmoja au miwili pale timu za taifa zinapokuwa zimecheza.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers