Hata mwezi haujaisha aliyekuwa kocha wa`mabingwa Kagame Dar Es Salaam Young African Tom Saintfiet amepata kazi tena sasa akiwa kocha mkuu wa Timu ya taifa ya yemen Mbelgiji huyo alionyeshwa kadi nyekundu baada kuanza vibaya katika ligi kuu ya soka ya vodacom licha ya kuwapa ubingwa wa afrika mashariki
.
Saintfiet, ambaye aliwahi kuwa mtaalamu wa ufundi katika nchi ya Ethiopia Ataanza kazi siku ya jumapili ambapo ataiongoza timu hiyo katika mechi ya kirafiki dhidi ya lebanon 16th October.
Ni kweli mimi ni kocha wa timu ya taifa ya yemen nina furaha na nipo tayari kwa kazi hii mpya inaonesha kuwa ninauwezo Nina Amini kuwa nitapata jambo hapa na kwa kiwango cha timu ya taifa ya Yemen haitakuwa rahisi lakini nilisha thibitisha hapo nyuma na ni ukweli nilifanikiwa
“katika mechi yao ya hivi karibuni walifungwa na Morocco mabao manne kwa sifuri katika kombe la Timu za kiarabu mbelgiji huyu ana kazi kubwa ya kuitoa yemen katika nafasi ya 157th katika viwango vya ubora wa fifa
No comments:
Post a Comment