HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 November 2012

Bunjak ashangaa tuhuma za rushwa Azam


Kocha aliyedumua Azam kwa siku 84 kabla ya kutimuliwa kufuatia kipigo cha magoli 3-1 walichokipata kutoka kwa Simba wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mserbia Boris Bunjak, ameelezea kushangazwa kwake na taarifa za kusimamishwa kwa nyota wanne wa timu yake hiyo ya zamani kwa tuhuma za rushwa.

Azam imewasimamisha kipa Deogratias Munishi ‘Dida’ na mabeki Erasto Nyoni, Said Morad na Aggrey Morris kwa tuhuma za kupokea rushwa na kuihujumu timu yao katika mechi dhidi ya Simba.

 Akizungumza na Chanzo chetu  kutokea kwao Serbia jana, Bunjak alisema ameshtushwa na taarifa hizo kwa sababu alikuwa karibu sana na wachezaji hao na hakutegemea kama wanaweza kukumbwa na tuhuma nzito kama hizo.

“Niko hapa Serbia na Boban Torlakovic (aliyekuwa kocha wa makipa wa Azam kabla hawajatimuliwa pamoja)… tunafuatilia kinachojiri katika klabu ya Azam, hasa ukizingatia kuwa tumeondoka kwa kusitishiwa mikataba,” alisema Bunjak.

“Tumepata taarifa siku tano zilizopita kwamba Azam ina matatizo makubwa na baadhi ya wachezaji wake. Tumesikia wengine wamehusishwa na rushwa… ni jambo la kushangaza sana kwa sababu Azam inalipa vizuri na inalea vizuri wachezaji wake.

“Hatuwezi kusema sana kwa sababu kila nchi ina tabia zake, labda hilo ndilo soka la Tanzania,” alisema Bunjak.
“Ni kweli katika mechi ya Simba timu yetu ilicheza vibaya, lakini mimi na rafiki yangu hapa (Torlakovic) hatukufikiria hata kidogo kwamba wachezaji walituzunguka kwa wapinzani wetu na kugawa ushindi.

“Nafikiri tuache uchunguzi ufanywe ili kujua ukweli wa jambo hilo… inasikitisha sana mchezaji wa klabu yenye mipango mikubwa kama Azam kuhusika na kitendo cha namna hiyo. Ni vigumu kuamini,” alisema.

Torlakovic, ambaye alitimuliwa Azam baada ya wiki mbili tu, alisema kuwa amesikitishwa na taarifa hizo za Azam ambao wamemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo wakiwa katika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi pointi 24 katika mechi 13 walizocheza.

“Tuliambiwa wachezaji watatu, baadaye tukaambiwa wanne wamesimamishwa baada ya kutuhumiwa kuuza timu kwa wapinzani,” alisema Torlakovic bila kutaja aliyewapa taarifa hizo.

“Haikuwa rahisi kuamini taarifa hizo... Azam na mamlaka za soka za nchi zichunguze kwa umakini na kukemea vitendo hivyo maana ni hatari kwa maendeleo ya soka.

“Hili si jambo jema na litawarudisha nyuma Azam katika mipango yao. Huwezi ukawa na timu bora katika hali ya migogoro na rushwa. Wasalimie Tanzania.”

Uongozi wa Azam ulitangaza kuwaweka kando nyota wake hao wa kikosi cha kwanza wiki iliyopita ili wapishe uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

Maamuzi hayo yalionekana kuiathiri timu yao katika mechi zake mbili za kufunga mzunguko wa kwanza kwani ilijikuta ikipata ushindi wa nyumbani wa goli 1-0 dhidi ya JKT Oljoro kabla ya kupoteza mechi ya mwisho kwa kufungwa 2-1 dhidi ya JKT Mgambo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers