HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 November 2012

Tanzania Kama kawaida yetu


Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya wazi katika mchezo wa vishale ya Kenya Open yaliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya wamerejea mikono mitupu huku wenyeji wakitwaa mataji ya michezo yote.

Michezo ilifungwa rasmi jana na kushuhudia Magereza Kenya wakitamba kwa kunyakua ubingwa wa Kenya Open kwa upande wa wanaume na wanawake, wakati timu ya ICC Arusha yenye wachezaji Joyce Mollel na Elizar Christopher wakifanikiwa kuifuta machozi timu dhaifu ya Darts Tanzania kwa kuambulia nafasi ya pili.

Katika michezo inayokutanisha mchezaji mmoja-mmoja, wawili-wawili na timu, kwa wanaume na wanawake, kote Tanzania ilitoka kapa.

Akitoa tathmini ya mwenendo mzima wa mashindano ya mwaka huu ya, katibu mkuu wa Chama cha Darts Taifa (TADA), Kaale Mgonja, alisema sababu za timu ya Tanzania kufanya vibaya katika mashindano hayo ni kukosa maandalizi ya kutosha kutokana na kukosa udhamini wa vifaa vya mazoezi.

“Mashindano yalikuwa mazuri, wenzetu ni tofauti na sisi walionesha kujiandaa. Sisi timu yetu ilikosa maandalizi mazuri kutokana na upungufu wa vifaa, hatukupata sapoti yoyote kutoka kwa serikali wala udhamini zaidi ya juhudi zetu binafsi na nawapongeza vijana wetu kwa kazi kubwa waliyoifanya,” alisema Mgonja.

Alisema wanategemea kurejea nchini kesho kujiandaa na mashindano yajayo, ambapo alisema kuwa klabu zote zitarejea katika kambi zao kujifua kwa maandalizi ya michezo ya Uhuru Safari yatakayofanyika kuanzia Desemba jijini Dar es Salaam kabla ya yale ya kimataifa ya majiji (Darts Inter City Challenge) yanayotarajiwa kufanyika Aprili mwakani jijini Nairobi.

Tanzania iliwakilishwa na timu sita kutoka katika mikoa minne ambazo VIP, ICC na Magereza (Arusha), Kimanga (Dar es salaam), Magereza (Kilimanjaro) na Ilemela (Mwanza)

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers