HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 November 2012

KAMATI IBRAHIM MAESTRO YAFUTWA

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amevunja Kamati zote tano za klabu hiyo alizoziunda wakati akiingia madarakani miaka miwili iliyopita baada ya timu kufanya vibaya kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Bara.

 Rage amesema amefikia maamuzi hayo baada ya kukutana na kamati ya utendaji juzi.

 Rage amesema kuwa amefikia hatua ya kuvunja kamati hizo tano kwa sababu ameona hazijafanya kazi yake ipasavyo.
 Kamati hizo ni ya Ufundi iliyokuwa ikiiongozwa na Ibrahim Masoud 'Maestro', kamati ya mashindano iliyokuwa chini ya Joseph Itang'ala 'Kinesi' pamoja na kamati ya nidhamu iliyokuwa ikiongozwa na Peter Swai.
 Pia Rage, amesema kuwa ameifuta pia kamati ya fedha iliyokuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu', na kamati ya usajili iliyokuwa chini ya Zacharia Hanspope.
 "Nimetumia nguvu yangu kikatiba kuzivunja kamati hizi kwa lengo zuri tu la kujipanga upya kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu," alisema Rage.
 "Kama ambavyo wanachama wameona, mzunguko wa kwanza hatujafanya vizuri na hii imetuumiza wanasimba wote.
 "Naenda nyumbani Tabora kutuliza kichwa na kuchagua watu wengine kuongoza kamati hizi.
 "Wanasimba watulie kwa kuwa tunajipanga sasa kwa ajili ya mzunguko wa pili."
 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers