HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 November 2012

MKINILIPA NA RUDI!!!


 kocha wa zamanai  wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba, Mganda Moses Basena amesema  bado timu hiyo haijamlipa haki yake lakini yuko tayari kurejea Dar es Salaam kuifundisha endapo watamlipa fedha anazowadai.

Simba iliamua kuachana na Basena mwaka jana baada ya kuona timu haichezi vizuri na kuamua kumchukua Mserbia Milovan Cirkovic, ambaye naye kwa sasa amekalia kuti kavu.

 Basena amesema kwamba anafahamu 'siasa' za soka la Tanzania hasa za Simba na Yanga hivyo hana kinyongo cha kurejea kuifundisha timu hiyo kwa mara ya pili endapo watakaa na kukubaliana upya na viongozi wa klabu hiyo.

 Basena ambaye sasa anaifundisha timu ya Express iliyoko kwenye nafasi ya 9 kati ya timu 12 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Uganda amesema anaamini akirejea ataifanya Simba iwe na makali yake.

"Nimesikia sasa timu iko katika hali mbaya, mimi waliniacha lakini niliwaacha wakiwa vizuri, sikuwahi kupata matokeo mabaya kama yaliyopo hivi sasa, mimi najua kazi yangu ila siasa ndizo zilizoniondosha, na walinipa tiketi ya kuja nyumbani (Kampala) na kurudi kazini (Dar es Salaam)" alisema kocha huyo ambaye alipewa taarifa za kufukuzwa kazi kwa njia ya barua pepe.

Aliongeza kwamba endapo yeye atapewa timu hiyo ana uwezo wa kuifanya Simba itetee ubingwa wake kwa kushinda mechi za mzunguko wa lala salama ambao utaanza mapema mwezi Januari mwakani.

"Na kikubwa ni kuanza maandalizi mapema ili timu iwe tayari kushindana katika mashindano ya kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika," alisema kocha huyo ambaye kabla ya kujiunga na Simba alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Uganda (Cranes).

 Aidha amefurahi kukutana na wachezaji wake wa Simba walioko katika kikosi cha timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakiongozwa na nahodha Juma Kaseja na kuwataka wacheze kwa bidii kwa sababu timu zote zimejiandaa na hakuna mwenye mteremko katika michuano hii ya Kombe la Chalenji inayoendelea.

Simba imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ikiwa katika nafasi ya tatu, pointi sita nyuma ya watani zao Yanga walio kileleni huku wakifuatiwa na Azam iliyo katika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers