Ni raha tupu kwa wachezaji wa Ashanti
Timu ya soka ya Ashanti wameichapa Villa Squad mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa katika uwanja wa Karume, jijini Dar es salaam.
Ashanti walipata bao la kwanza dakika ya nne mchezo kwa goli la Jerome Lembeli bao lililodumu hadi nusu ya kwanza inamalizika.
Dakika ya 59 Villa Squad walipata pigo baada ya mchezaji Raymond Zablon kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea kwa makusudi mchezaji wa Ashanti United akiwa bila ya mpira .

katika Dakika ya 88 ya kipindi cha pili Jerome Lembeli tena alifunga bao la pili na kuhakikishia timua yake ushindi katika mechi hiyo .
katika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani Wanajeshi wa JW Green Warriors waliibamiza Transit Camp kwa bao 1-0 kwa goli lililofungwa na Zamkufo Elius dakika ya 40 kwa maana hii Ashanti inaendelea kuongoza kundi B baada ya kucheza michezo mitano na kufikisha pointi 15
Kundi A, Mjini Iringa Polisi Iringa wameifunga Burkina Fasso ya Morogoro mabao 2-0.
Mabao yamefungwa na Dimosi Malisa dakika ya 53 na Japhet Mamboleo dakika ya 57.

No comments:
Post a Comment