HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 December 2012

AAAAAHH HACHEZI ULAYA HUYU!! :KATONGO

Nahodha wa timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika, Christopher Katongo na beki wa kikosi cha wachezaji 11 wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Stopilla Sunzu Walishangaa kusikia  winga Mrisho Ngassa wa timu ya taifa (Taifa Stars) anacheza  soka la ridhaa ndani ya Tanzania licha ya kuonyesha kiwango cha juu na kufunga goli pekee lililowazamisha katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.

  Nyota hao walioshindwa kuisadia Zambia isilale kwa goli 1-0 juzi, wamesema kuwa Ngassa anastahili kucheza nje ya Tanzania kutokana na uwezo alio nao.

“Yule mchezaji mwenye jezi namba nane (Ngassa) ni hatari sana. Anazijua njia za mpira na ana kasi sana,” alisema Sunzu, ambaye kaka yake Felix Sunzu anaichezea Simba ya Tanzania.

 Sunzu aliongeza kuwa Ngassa aliwapa tabu katika eneo la safu ya ulinzi katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kutokana na uwezo wake wa kukimbia kwa kasi huku pia akiwa mzuri kwa chenga; na anaamini kwamba akipata nafasi anaweza kufanya makubwa akiwa nje ya Tanzania.

Katongo pia alimsifu Ngassa na kusema kuwa awali, alidhani ni miongoni mwa nyota wachache wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.


“Yule (Ngassa) ni mchezaji mzuri sana. Nimeshangaa nilipoambiwa kwamba anacheza hapa hapa Tanzania na nilifikiri anacheza nje ya hapa,” alisema Katongo.

 Ngassa ‘aliwaua’ Zambia kwa kufunga goli pekee katika dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers