HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 December 2012

Brendan Nataka kuongeza kandarasi ya Gerrard

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema anataka kuongeza muda wa kandarasi ya nyota wake Steven Gerrard ambaye pia ni naodha wa klabu hiyo akisema kuwa mchezaji huyo bado angali na majumu mengi katika klabu hiyo.

Mkataba wa Gerrard na Liverpool unamalizika mwisho wa msimu ujao na kocha huyo anasema bado anataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na mbili kuendelea kuichezea klabu hiyo.

 kiungo huyo wa uingereza  amefunga magoli 153 baada ya kuichezea Liverpool mechi 609.

Gerrard alisajiliwa na Liverpool mwaka wa 1998 na aliiongoza klabu hiyo kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka wa 2004-05.

Naodha huyo pia aliiongoza Liverpool kushinda komeb ha FA mara mbili, kombe la ligi mara tatu na kombe la EUFA.

Gerrard amecheza mechi zote la Ligi tangu kocha mpya wa klabu hiyo Brendan Roggers kuteuliwa mwanzo wa msimu huu, na amefunga bao katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Aston Villa na Fulham.

Mwaka wa 2004, Steve Gerrard alikataa kukihama klabu hiyo, ikiwa na pamoja na mpango wa Chelsea wa kumsajili mwaka wa 2004.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers