Zanzibar Heroes, mabingwa wa mwaka 1995 ambao katika mchezo wa robo fainali ya pili wamefanikiwa kuwafunga Burundi (Intamba Murugamba) kwa penati 6-5 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika bila kufungana.Abdallah Othman alifunga penati ya ushindi kwa Zanzibar baada ya Fiston Abdoul wa Burundi kupoteza penati yake
Nahodha wa Burundi Selemani Ndikumana na nahodha Zanzibar Nadir ‘Cannavaro’ Haroub walokosa penati zao.
Ndani ya dakika 90 mshambuliaji wa Zanzibar Juma Jaku Juma alipoteza nafasi nyingi za kumalizia huku mlinda mlango Ally Mwadini akiokoa mipira mingi iliyo elekezwa langoni kwake na Selemani Ndikumana na Christopher Nduwagira.
Penati za Zanzibar zilifungwa na Khamis Mcha Khamis, Adeyom Saleh Ahmed, Juma Jaku Juma, Nuhu Haji Samih, Aggrey Morris na Abdallah Othman wakati ambapo kwa upande wa Burundi penati zao zilifungwa na Styve Nzigamasabo, Amisi Tabwe, Christopher Nduwagira, Leopold Nkurikiye na Gael Duhatindayishimiye.

No comments:
Post a Comment