HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 December 2012

Kluivert :RONALDO UNA BAHATI MBAYA KUCHEZA NYAKATI MOJA NA MESSI



Kocha wa Arsenal ,Arsene  Wenger amesema kuwa bado hajaghairisha mpango wake wa kutaka kumsajiri kwa mara ya tatu mchezaji wa zamani wa timu hiyo  Thierry Henry kwa mkataba wa muda mfupi 

 Mfaransa ambaye alifunga magoli matatu  ,katika mechi saba msimu uliopita akitokea  New York Red Bulls, amekuwa akifanya mazoezi tangu msimu wa ligi huko marekani ulipokwisha 

lakini wenger anaamini kuwa bado atambakisha theo walcot ambaye kandarasi yake inaisha mwezi wa sita na bado hajatia saini kandarasi nyingine aidha wenger amesitisha mpango wa kutaka kumsajiri Demba Ba kutoka Newcaslte utd huku akijibu swali aliloulizwa  unampenda ba ndio vp mtamsajiri :-wenger alijibu hapana 

RONALDO UNA BAHATI MBAYA KUCHEZA NYAKATI MOJA NA MESSI

Mchezaji wa Zamani wa Timu ya taifa ya uholanzi na Barcelona ya uispania Patrick  Kluivert  amemwambia kijana wa kutoka ureno Cristaino Ronaldo kuwa ana bahati kucheza nyakati moja na Lionel Messi .

Huku kukiwa kumesaria majuma kadhaa ya kumtangaza mchezaji wa atakayetwaa tuzo ya  Ballon d'Or  messi anapigiwa zaidi chapuo kutwaa tuzo hiyo huku akiwa amevunja takwimu ya gwiji la soka la ujerumani Gerd Muller' kwa kufunga magoli mengi zaidi kwa mwaka  

Mchezaji huyo mstaafu wa uholanzi ambaye alichezea klabu hiyo kwa miaka sita anaamini kuwa mchezaji huyo sio tu kuwa ni bora  ukimfananisha na mwenzake wa Real Madrid 
 Cristiano Ronaldo kwa kugombania tuzo hiyo kwa pamoja .

"Cristiano Ronaldo ni mzuri  , lakini anabahati mbaya kwa kucheza nyakati moja na messi aliambia (Mundo Deportivo) yaani ulimwengu wa michezo .

"Je messi ni mchezaji bora wa muda wote ?Binafsi , Ndio."

Andres Iniesta, Ronaldo na  Messi watapambana katika kuwania tuzo hiyo ya mwanasaoka bora wa Dunia  Ballon d'Or  2013.

Pardew ATAKA FA KUMFUNGIA Ferguson

Kocha wa Newcastle United  Alan Pardew anahisi kocha mwenzake wa Manchester United  Sir Alex Ferguson anatakiwa kupewa adhabu baada ya kumghasi mwamuzi msaidizi katika mechi ya ligi kuu ya uingereza ilichezwa siku ya shamra shamra ya ufunguaji zawadi baada ya krismasi maarufu kama  Boxing Day.

 Sir Alex alikuwa anambwatukia kwa hasira  Mike Dean's baada ya kuingilia maamuzi ya mwamuzi msaidizi  Jake Collin's ambaye aliashiria kuotea kwa Ba  na badala yake  Jonny Evan's kujifunga mwenyewe katika mechi ambayo United  ilishinda  4-3 Dhidi ya  Magpies.

Waamuzi hawakumpa adhabu yoyote na vilevile katika taarifa yao baada ya mechi hawakuzungumzia  kabisa tukio hilo

 lakini  Pardew anafikiri kuwa  FA bado inatakiwa kuchukua hatua ya zaidi.

Pardew pia amesema kuwa tazama hata  FA imeshindwa kumpa adhabu  Robin van Persie' ambaye alimjeruhi kwa makusudi  Fabricio Coloccini.

Aliongeza : "Nadhani kulikuwa na mambo mengi ambayo FA
ilitakiwa kutazama lakini inaonekana hawatatazama lolote ."

Malalamiko haya ya Pardew's yanakuja baada ya  FA' kuamua kuchunguza kauli za makocha wawili akiwemo wa  Manchester City  Roberto Mancini na  QPR  Harry Redknapp baada ya timu hizo kufungwa dhidi ya Sunderland na  West Brom.

Mancini alisema

"Labda waamuzi walikula sana siku ya  Christmas," Mancini .
Akilalamika baada ya zabaleta kufanyiwa madhambi ambayo waamuzi hawakuiona na kusabisha kufungwa goli moja  bila dhidi ya Sunderland

Wakati Redknapp, alimkebehi mwamuzi kuwa ana matatizo ya kutokuona vizuri baada ya mchezaji wa west brom kuunawa mpira na ushindwa kuzawadiwa Penati na hivyo kufungwa 2-1

"Labda angeenda kutizama macho ya kwenye mashine ya kutizamia ugonjwa macho kafanya maamuzi ya kashfa kabisaa alimaliza Harry "

Galliani:Athibitish kutaka kumuuuza  Robinho santos  

Wakuu wa timu ya  Rossoneri kwa sasa wapo amerika ya kusini wakiwa wanafanya makammilisho ya uhamisho wa mchezaji wa timu na mshambuliaji wa nguli wa AC Milan  Alexandre Pato,

lakini Raia mwenzake wa Brazil ni moja kati ya wachezaji wengine ambao wataweza kuuzwa katika dirisha dogo la mwezi  January.


Makamu wa Rais wa klabu hiyo Galliani amethibitisha kuwa mchezaji wa zamani wa Real Madrid Robison De souza ,
naye atauzwa huku akikiri kuwa  Flamengo haijaonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ambaye alianza maisha ya soka  miaka kumi iliyopita akiwa  Santos 10 .

"Kuna uwezokano wa kumuuuza santos galiani aliambia  Globo Esporte. "Bado hautajafika maamuzi na  Flamengo, nafikiri wakati huu bado hatujui kuhusu  Atletico Mineiro."

Pato's huenda akarejea kwao mwezi january ,Huku corithians ikionyesha kuvutiwa na  Robinho' , Japokuwa bado haijafahamika atakwenda sehemu gani , Makamu wa Rais wa  Sao Paulo :- Joao Paulo de Jesus Lopes amethibitisha timu yake imekataa kutaka kumsajiri mchezaji huyo mwenye miaka  28-.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers