Kilimanjaro Stars imefuzu Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CECAFA , baada ya kuilaza Somalia mabao 7-0 katika mchezo uliofanyikakwenye Uwanja wa Lugogo .
Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu, wakishinda mbili na kufungwa moja.
Iliwachukua sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC, Mrisho Khalfan Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.
Kabla hawajakaa vizuri, Somalia walipachikwa bao la pili, dakika ya 23 lililofungwa na Ngassa tena, aliyeunganisha kona ya Issa Rashid.
John Bocco ‘Adebayor’ alifunga bao la tatu katika mchezo huo na la tatu kwake katika mashindano hayo dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid kutoka wingi ya kushoto.
Bocco tena aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa, akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.
Ngassa alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’
Somalia ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na Hussein Abdallah.
Kipindi cha pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74 pasi ya Ramadhani Sinago.
Kwa kufunga mabao matano, Ngassa sasa ameingia kwenye mbio za kiatu cha dhahabu akiwa anaongoza, akifuatiwa na Bocco ambaye ana magoli manne .

No comments:
Post a Comment