HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 September 2012

SUNDERLAND 1-1LIVERPOOL




Luis Suarez equalises for Liverpool at Sunderland


ESPERANCE YASHINDWA KUWEKA REKODI


 

Klabu ya soka kutoka  Tunisia Esperance imeshindwa kutetea rekodi yake ya kutopeteza mechi katika ligi ya mabingwa barani afrika baada ya kufungwa goli moja kwa sifuri Dhidi ASO Chlef kutoka Algeria jana Ijumaa 
 Mchezaji wa kimataifa wa cameron  Anicet Eyenga alicheza vizuri na kufunga goli safi katika mwa kipindi cha kwanza cha  mchezo huo na kuitimisha kabisa rekodi ya Esperance ya kutokufungwa takriban mechi 19 Esperance walitakiwa kukwepa kipigo ili kuwapiku mabingwa mara sita Al Ahly ya Misri ambao nao walicheza mechi  19 bila kufungwa katika miaka ya 2004 na 2006
 Vijana hao kutoka  Tunisia  waliwapiku  Ahly baada ya kuwafunga  Etoile Sahel mwezi uliopita ,lakini matokeo yao yalifutwa baada ya kutokea fujo kiwanjani baada ya kufungwa na ASPAC ya  Benin mwezi  April, vijna hao ambaoo damu ya ushindi ilikuwa imechanganya kwa mng'ao wa dhahabu walikuwa hawajafungwa katika mechi 12 ilikutwaa ubingwa kwa mara ya pili  waliwafuata katika uwanja wao nyumbani  Chlef bila ya kufungwa  katika mechi saba za kufuzu kwenye makundi  msimu huu . ukiachana na kutengeneza rekodi ,ni timu mbili ambazo zimekamata mnofu wa kucheza nusu fainali ya klabu bingwa afrika  ambapo ni wenyewe Esperance na  Sunshine Stars kutoka  Nigeria ambazo tayari zimeshatinga hatua ya nusu fainali   kundi  A na  Chlef ambayo tayari imesukmwa nje ya michuano kwa kushika nafasi ya mwisho baada ya kupata vipigo vitatu mfululizo 
Ahly na  mabingwa mara nne  TP Mazembe kutoka Jamhuri ya kidemocrasia ya watu wa congo ndio zimefuzu kucheza hatu ya nusu fainali katika kundi B na kesho jumapili itacheza ilikujua nani anamaliza kuwa kiongozi wa kundi hilo ili kuikwepa Esperance. Mazembe inaongoza  Ahly katika mechi zilizokutanisha timu hizo ambapo itamaliza ya kwanza kama itaifunga Berekum Chelsea ya  Ghana wakati  Ahly itakwaana mabingwa wa Karne huko   Cairo dhidi ya  Zamalek mechi zitachezwa muda mmoja

 

MWANZO MZURI





Ligi kuu ya Tanzania Bara imeanza hii katika viwanja saba tofauti hapa nchini , ambapo mabingwa watetezi wa taji, Simba walikuwa katika uwanja wa taifa ikifungua pazia la ligi dhidi ya Afrikan Lyon imechomolza na ushindi wa mabao 3-0.
Simba imepata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji hatari Emmanuel Okwi bao lililopatikan katika kipindi cha kwanza kabla ya bao la pili kuwekwa wavuni na mlinzi wa kulia Nassoro Cholo.
Bao la tatu lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia kwa njia ya penati baada ya walinzi wawili wa Lyon kumkwatua Emmanuel Okwi katika eneo la hatari na bao hilo kuzamishwa wavuni na mshambiliaji Daniel Akufor.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Simba Milovan Circkovic amesema ameridhishwa na kiwango cha timu yake huku akipongeza kikosi chake kwa kuanza ligi hiyo na matokeo hayo.
Amesema anatarajia nidhamu ya kimchezo iliyoonyeshwa na kikosi chake itaendelezwa katika mchezo unaofuata ambao Simba itakuwa ikicheza dhidi ya JKT Ruvu mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Taifa.
Matokeo mengine mabingwa wa kombe la Kagame Yanga wamekwenda sare ya bila mabao 0-0 na Tanzania Prisons mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine pale mkoani Mbeya.

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akikokota mpira huku mchezaji wa Jacob Massawe akimnyemelea wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi ambapo Simba ilishinda bao 3-0 Dhidi ya African Lyon . 

ROCKERSPORT UNDSTAND

KITAALAMU ZAIDI


MSIMAMO LIGI YA PREMIER UINGEREZA


ZANZIBAR KWAANZA KUFUKUTA

BAADA ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya soka Zanzibar kwa kuchapwa magoli 2-0 na Jamhuri, klabu ya Duma imemgeukia mwamuzi wa pambano hilo Ali Omar Kisaka, ikidai aliwapa wapinzani wao penelti kwa kushawishika na zogo la mashabiki.
 
Kocha wa wajenga uchumi hao Asaa Khamis, amesema katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Gombani, penelti ya kwanza haikuwa sahihi, na kwamba hakufikiria kama mwamuzi engelishawishika na kelele za mashabiki wa Jamhuri hasa kwa vile alikuwa mbali na eneo lililotokezea kadhia hiyo, ingawa baadae aliamuru ipigwe penelti. Wakati huo huo
MATARAJIO ya wadau wa soka wa Zanzibar kupumua baada ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kupata Rais mpya, yameanza kuingia doa kutokana na kuwepo dalili za mvutano mpya unaoelekea kuchipua.
 
Hali hiyo imebainika baada ya Kamati Tendaji ya chama hicho kisiwani Pemba, kudai kuwa haishirikishwi na wenzao wa Unguja, wakiwalaumu kwa kuchukua maamuzi mazito na ya kitaifa  peke yao.
 
Kamati hiyo ya Pemba, ilifanya kikao Septemba 11 kujadili utendaji dhaifu unaofanywa na Kamati Tendaji ya ZFA Taifa ya Unguja, na kutoa azimio la kutoyatambua maamuzi yote yaliyochukuliwa na kamati hiyo hivi karibuni.
 
Maamuzi hayo yamepelekwa kwa Kaimu Rais wa ZFA Haji Ameir Haji, na Zanzibar Leo  kupata nakala yake.

VODACOM PREMIER LEAGUE



 Simba    3 VS      0     African Lyon

Toto 1 jkt oljoro 1

Polisi Dodoma 0  VS0    Mtibwa Sugar
, Mgambo JKT   0   VS 1 JERY SANTO  Coastal Union.

Tanzania Prisons 0  VS  O  Yanga.MBEYA

  
JKT Ruvu  2  VS1   Ruvu Shooting


  Azam  1 TAIGA   VS 0    Kagera Sugar

LIGI KUU YA SOKA YA PREMIER YA UINGEREZA

Anton Ferdinand and John Terry 
Tushikane mikono kaka 
QPR 0 - 0 Chelsea FT

 
Arsenal 6 - 1 Southampton FT
  Javi Garcia scores for Man City 
 

Peter Crouch celebrates 
Nimesawazisha
 Javier Hernandez misses penalty 
 Man Utd 4 - 0 Wigan FT

Paul Scholes 
PAUL BADO YUPO FIT
 
Dimitar Berbatov celebrates

Matthew Lowton's swerving shot beats Swansea keeper Michel Vorm 


 Joey O'Brien tangles with Robert Snodgrass 


 

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers