HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 September 2012

ZANZIBAR KWAANZA KUFUKUTA

BAADA ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya soka Zanzibar kwa kuchapwa magoli 2-0 na Jamhuri, klabu ya Duma imemgeukia mwamuzi wa pambano hilo Ali Omar Kisaka, ikidai aliwapa wapinzani wao penelti kwa kushawishika na zogo la mashabiki.
 
Kocha wa wajenga uchumi hao Asaa Khamis, amesema katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Gombani, penelti ya kwanza haikuwa sahihi, na kwamba hakufikiria kama mwamuzi engelishawishika na kelele za mashabiki wa Jamhuri hasa kwa vile alikuwa mbali na eneo lililotokezea kadhia hiyo, ingawa baadae aliamuru ipigwe penelti. Wakati huo huo
MATARAJIO ya wadau wa soka wa Zanzibar kupumua baada ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kupata Rais mpya, yameanza kuingia doa kutokana na kuwepo dalili za mvutano mpya unaoelekea kuchipua.
 
Hali hiyo imebainika baada ya Kamati Tendaji ya chama hicho kisiwani Pemba, kudai kuwa haishirikishwi na wenzao wa Unguja, wakiwalaumu kwa kuchukua maamuzi mazito na ya kitaifa  peke yao.
 
Kamati hiyo ya Pemba, ilifanya kikao Septemba 11 kujadili utendaji dhaifu unaofanywa na Kamati Tendaji ya ZFA Taifa ya Unguja, na kutoa azimio la kutoyatambua maamuzi yote yaliyochukuliwa na kamati hiyo hivi karibuni.
 
Maamuzi hayo yamepelekwa kwa Kaimu Rais wa ZFA Haji Ameir Haji, na Zanzibar Leo  kupata nakala yake.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers