Timu ya Azam FC imewasili salama jijini Nairobi nchini
Kenya jana usiku tayari kwa kuanza michezo yake wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya
maandalizi kwa ajili ya ligi kuu ya Tanzania mzunguko wa pili pamoja na
mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumzia program nzima ya maandalizi kocha wa
Azam FC, Stewart Hall amesema timu itacheza mechi tatu za kirafiki na kufanya
mzoezi ya siku mbili katika viwanja vya Nyayo na City.
Alisema wachezaji wote wamefika salama, timu
itaacheza mchezo wake wa kwanza kesho ‘Jumamosi’ saa 3:30 (15:30hrs) dhidi ya
A.F.C Leopard, kwenye Uwanja wa Nyayo.
Azam FC leo ‘Ijumaa’ jioni itafanya mazoezi yake ya
kwanza katika Uwanja wa Nyayo uliopo katikati ya jijini la Nairobi.
“Tutacheza michezo mitatu, michezo yetu itahusisha
timu zenye viwango vizuri katika ligi ya Kenya ambazo ni A.F.C Leopard,
Sofapaka na K.C.B, mechi hizo zitasaidia kuimarisha timu yangu” alisema
Stewart.
Kocha Stewart alisema watafanya mazoezi na kucheza
mechi katika viwanja aina mbili vyenye nyasi za kawaida na zenye nyasi bandia
kwa kuwa katika michezo ya ligi viwanja hivyo vinaendana na mazingira ya
Tanzania.
Azam FC iliyoko nchini hapa bila ya washambuliaji
wake John Bocco na Tchetche Kipre na mchezaji Waziri Salum wanaosumbuliwa na
majeruhi, siku ya Jumapili itacheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya
SOFAPAKA kwenye uwanja huo huo.
Baada ya mchezo huo kikosi hicho kitapumzika siku ya
Jumatatu Jan 21, 2013 ambapo watatumia siku hiyo kufanya mazoezi katika Uwanja
wa City wenye nyasi bandia.
Azam FC itamaliza safari yake ya maandalizi na mechi
za kirafiki siku ya Jumanne Jan 22 ambapo watacheza dhidi ya K.C.B kwenye
Uwanja wa City mchezo ambao utakamilisha safari hiyo ya siku saba.
Wachezaji walioko jijini ni Mwadini Ally, Aishi
Manula, Jackson Wandwi, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Luckson
Kakolaki, Jockins Atudo, Michael Bolou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence
Mwaikimba, Uhuru Selemani, Brain Umony, Malika Ndeule, Omary Mtaki, Abdi Kassim
‘Babi’, Abdalah Seif, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Contacts
Ass. Manager Jemedari Said
+255 713528790
Azam FC Program
17th Players Arrive
18th Team Training at Nyayo Stadium 4:00
PM
19th Game vs A.F.C Leopard- Nyayo Stadium
3:30PM
20th Azam FC vs SOFAPAKA –Nyayo Stadium
3:30PM
21st Training at City Stadium 4:00 PM
22nd Game vs K.C.B-City Stadium 4:00PM
No comments:
Post a Comment