MFANYABIASHARA maarufu hapa nchini, Yusuf Manji, ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, amerudisha fomu Ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) leo, huku nafasi hiyo ikiombwa na watu watatu na uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Februari 22 mwaka huu.
Kama kawaida, Manji alirudisha fomu akiongozana na mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Zamunda, wakati leo wakijitokeza wengine kuchukua fomu wakiomba ujumbe wa Bodi kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza.
Orodha ya waombaji uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuf Manji wa Yanga wanaoomba uenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Kwa upande wa wajumbe wawili kuwakilisha klabu za Daraja la Kwanza ni Christopher Peter Lunkombe wa Moro United ya Dar es Salaam na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza.
No comments:
Post a Comment