Raia wa Brazil wanaomboleza vifo vya wenzao 233
waliokufa kwenye klabu ya usiku katika mji mdogo wa
Santa Maria, usiku wa kuamkia jana. Zaidi ya watu 100
walijeruhiwa kwenye mkasa huo wa kutisha, huku miongoni
mwa waliookoka wakielezea namna wenzao walivyonasa
kwenye jengo la klabu hiyo ya Kiss lililokuwa na mlango
mmoja tu wa kutokea na kufa kwa kupaliwa na moshi na
mkanyagano. Wengi wa waliokufa na majeruhi wanahofiwa
kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Waziri wa Afya, Alexandra
Padilha, amewaambia waandishi wa habari kwamba kwa
sasa serikali yake inajaribu kuokoa maisha ya wale
inaoweza. Rais Dlima Rousseff aliyeripotiwa kuguswa vibaya
sana na mkasa huo, amekatisha ziara yake nchini Chile na
kurudi nyumbani, na serikali yake imefuta uzinduzi wa siku
500 kueleekea Kombe la Dunia linalochezwa mwakani nchini
humo, ambao ulikuwa ufanyike leo
No comments:
Post a Comment