1. Kamati
ya Uchaguzi ya TFF inawaarifu wadau wa soka kuwa kutokana na makosa ya
uchapaji, pingamizi iliyowekwa na Nd. Paul Mhangwa dhidi ya maombi ya
kugombea uongozi TFF ya Nd. Mugisha Galibona na Nd. Vedastus F.K.
Lufano, wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kupitia Kanda ya 2 (Mara na Mwanza) haikuchapishwa kwenye taarifa kwa
vyombo vya habari iliyotolewa awali
leo (Januari 27, 2013). Mnaarifikuwa kuwa Nd. Mugisha Galibona na Nd.
Vedastus F.K. Lufano wamewekewa pingamizi na Nd. Paul Mhangwa ambalo
lilipokelewa Januari 22, 2013.
2. Kamati ya Uchaguzi ya TFF itakutana Jumatano tarehe 30/01/2013
saa 4 kamili asubuhi kujadili pingamizi hizo. Waombaji uongozi
waliowekewa pingamizi na wawekaji pingamizi wanaarifiwa kufika kwenye
kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF tarehe 30/01/2013 saa 4 asubuhi
wanajulishwa kuwa barua za mwito wa kuhudhuria kikao hicho zimetumwa kwao kupitia
anuani za barua-pepe zilizoonyesha kwenye fomu za maombi ya uongozi na taarifa za pingamizi.
Angetile Osiah
Katibu
Kamati ya Uchaguzi TFF
No comments:
Post a Comment