African
Lyon ndiyo klabu iliyoongoza kwa kusajili wachezaji wengi kwenye
dirisha dogo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom
utakaotoa bingwa wa Tanzania Bara, lakini pia timu tatu ambazo msimu
ujao zitarudi kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
Kati
ya wachezaji 65 waliotua katika klabu mbalimbali katika dirisha hilo,
Lyon ndiyo iliyoongoza kwa kuwanasa 12. Miongoni mwao hao, wawili
(Ibrahim Job na Shamte Ally) imewachukua kwa mkopo kutoka Yanga.
Pia
watano imewapandisha kutoka katika kikosi chake cha U 20. Wachezaji hao
ni Nurdin Musa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na
jarufu Kizombi. Wengine walioingia katika timu hiyo katika dirisha dogo
ni Juma Seif (Huru), Buya Jamwaka (Burkina Faso), Takang Valentine
(Huru) na Yusuf Mgwao (Huru).
Nayo
Polisi Morogoro katika kuhakikisha inaondoka mkiani mwa ligi imesajili
wachezaji wanane katika dirisha dogo kama ilivyofanya Oljoro JKT ya
Arusha.
Wachezaji
wa kigeni walioingia katika dirisha dogo ni Humphrey Mieno, Brian
Umony, Jockins Atudo (Azam), Donald Obimma na Ulugbe Chika (Toto
Africans), Zuberi Hamis na Tinashe Machemedze (Coastal Union), Musa
Mudde na Abel Dhaila (Simba).
No comments:
Post a Comment