Hatimaye
Serikali imekubali kupunguza kiasi cha makato ya mapato ya michezo
inayochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na sasa itakuwa
ikichukua asimilia 15 tu ya mapato ya michezo yote itakayokuwa ikichezwa
katika uwanja huo.
Hayo
yamo ndani ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande tatu yaani
serikali, shirikisho la soka nchini TFF na bodi ya ligi makubaliano
ambayo yamesainiwa baada ya kikao cha wiki iliyopita.
Hii
leo katika ofisi za wizara ya habari, utamaduni na michezo huku
serikali ikiwakilishwa na naibu waziri Amos Makala na mkurugenzi wa
michezo Juliana Yasoda nayo TFF ikiwakilishwa na katibu mkiuu wake
Angetile Oseah na bodi ya ligi ambayo bado haijaundwa ikiwakilishwa na
afisa mtendaji mkuu wake Silas Mwakibinga yamesainiwa makubaloiano hayo.
Makubaliano
hayo sasa yatakuwa yanaleta unafuu kwa vilabu na timu za taifa ambazo
mara kwa mara zimekuwa zikiuutumia uwanja huo katika michezo ya ligi na
michuano ya kimataifa kwa ngazi mbalimbali.
Hata
hivyo bado maumivu ya makato ya uwanja huo yanaonekana kama yataendelea
kwa namna moja ama nyingine kwa kuwa bado kuna makato mengine
hayajapata nafuu yake kwa kuwa bado yatakuwa yakiendelea kama vile
makato ya gharaza za mchezo, maandalizi ya mechi, mashine za uwanjani ,
umeme na usafi pamoja na ulinzi bila kusahau chama cha soka mkoa
mwenyeji wa uwanja Dar es Salaam DRFA.
Akiongea
mbaele ya waandishi wa habari naibu waziri wa habari Amos Makalla
amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kilio cha muda mrefu na kwa
kuwa serikali ni sikivu imeamua kuchukua hatua hiyo muhimu kwa
kushirikiana na TFF na bodi ya ligi.
Kuhusu
suala la malipo ya fedha za makocha ambazo zimepelekea akaunti ya TFF
kuzuiliwa na mamlaka ya mapato nchiniTRA, Makalaa amesema suala hilo
linashughulikiwa na kwamba linakwenda vizuri likiwa katika hatua za
mwisho mwisho na kwamba kinacho subiriwa ni malipo ya kurudisha fedha
hizo kwenye akaunti iliyofilisiwa.
Pia amesema kwamba serikali itajitahidi jambo hilo lisijirudie tena.
Pia
Makalla amevipongeza vilabu vinavyoshiriki ligi kuu kwa kukubali
kuingia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu unaoanza hapo kesho licha ya
kwamba vinakabiliwa na mazingira magumu ya kutokuwa na fedha ambazo
zimefungiwa katika akaunti hiyo ambayo ni maalumu kutunza fedha za
vilabu zinazotoka kwa mdhamini wa ligi kampuni ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment