Timu
ya Taifa (Taifa Stars) itacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya
Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Januari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Stars
chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen inatarajia kuingia kambini jijini Dar
es Salaam keshokutwa (Januari 6 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika
Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Ethiopia
iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina
Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi
ya Zambia.
Katika
mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika
mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Mechi
hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya
mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la
Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.
Wachezaji
wanaotakiwa kambini ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye
nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki
ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa
Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na
Shomari Kapombe (Simba).
Viungo
ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba),
Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas
Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati
benchi la Ufundi lina Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma
Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na
Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
UCHAGUZI KWA WANACHAMA WA TFF
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF inatarajia kukutana leo mchana (Januari 4 mwaka huu)
ambapo pamoja na mambo mengine itapitia maendeleo ya uchaguzi kwa
wanachama wa TFF ikiwemo Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
Wanachama
wa TFF (vyama vya mikoa) wote wameshafanya uchaguzi ukiondoa mikoa ya
Rukwa na Katavi inayotarajiwa kufanya uchaguzi baadaye mwezi huu. Kwa
upande wa vyama shiriki ambavyo bado havijafanya uchaguzi ni Makocha
(TAFCA), Wachezaji (SPUTANZA), Waamuzi (FRAT) na Tiba ya Michezo
(TASMA).
Vilevile
Kamati ya Uchaguzi ya TFF baada ya kikao hicho huenda ikatangaza rasmi
mchakato wa uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka
No comments:
Post a Comment