Timu ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza
na timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika
mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football
-Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo
jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu
hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka
jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata
nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina
wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi
na kuwavutia.
Baada ya kuwa na
wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld
ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya
kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona
maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa
tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor
FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani
ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya
mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji
wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na
Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni
miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame
Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho
katika uwanja wa Selen Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji
wa Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo
mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja
hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika
mchezo huo.
Athumani Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza
waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Amrnini
Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani wanaendelea na mazoezi pamoja
na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.
Kuhusu
hali ya hewa leo haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani
wanaonekana kuimudu na mda mwingi kwa sasa kumekua na jua linalowaka
kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka mida ya jioni, kwa leo hali ya
hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni nzuri kabisa na jua
linawaka mda wote.
No comments:
Post a Comment