Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa klabu ya TP Mazmebe
ya Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo wako shakani tena kujiunga katika
kambi ya timu ya taifa (Taifa Stars) iliyoanza kambi jijini Dar es
Salaam jana kutokana na uwezekano wa kuwekewa ngumu na timu yao.
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Boniface Wambura, amesema kuwa tayari wameshajulishwa kwamba
Samatta na Ulimwengu walioitwa kikosini na kocha wa Stars, Mdenmark Kim
Poulsen hawawezi kuungana na wenzao hadi shirikisho hilo
litakapozungumza na uongozi wa Mazembe ili kupata idhini ya kuwatumia.
Stars imeingia kambini jana kujiandaa kwa mechi tatu za kimataifa za kirafiki, ikiwamo dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia.
Wote wawili waliwahi kukataliwa na Mazembe kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) iliyofanyika Kampala, Uganda na hivi karibuni walishindwa pia kuichezea Stars dhidi ya Zambia baada ya kutua nchini wakitokea Kongo wakiwa majeruhi.
"Bado hatuna uhakika wa kuwapata Samatta na Ulimwengu… ila tumeanza harakati za kuwaleta kitambo na tayari Sunday Kayuni (Mkurugenzi wa Ufundi TFF) amekwenda Kongo kuwaombea ruhusa,” .
Akieleza zaidi, amesema kuwa kambi ilianza jana na kuwahusisha wachezaji wengine isipokuwa wa Simba, Azam na Mtibwa zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi, Zanzibar na Yanga ambayo iko ziarani Uturuki.

No comments:
Post a Comment