HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

14 January 2013

YANGA KUJARIBU MAFUNZO YA UTURUKI JPILI



Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), klabu ya Yanga watapima makali waliyoyapata Uturuki kwa kucheza mechi mbili za kirafiki kuanzia Jumapili dhidi ya timu kutoka Afrika Kusini ‘Sauzi’ na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Yanga ambao walikuwa wameweka kambi ya wiki mbili mjini Antalya, Uturuki kujiandaa kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wamewasiri alfajiri ya Leo katika uwanja wa kimataifa wa  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo alfajiri.


 Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako amesema kuwa timu yao itacheza mechi hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Hata hivyo, Mwalusako amekataa kuzitaja timu hizo kwa madai kwamba bado wako katika mazungumzo na kwamba mambo yatakapokamilika, wataweka kila kitu hadharani.

Yanga inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mabingwa wa mwaka huu wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wanaokalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakiwa na pointi 25, moja zaidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba ambao wanaendelea na kambi yao nchini Oman kujiandaa kwa mzunguko huo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers