Timu ya soka ya Napoli
na mashabiki wa timu hiyo watavaa skafu nyeusi katika mechi ijayo ikiwa ni ishara ya kumuaga mchezaji wa zamani wa timu ya Napoli ya italia aliyefariki akiwa na umri wa miaka 87.
katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu hiyo leo hii . Djurgarden, amethibitisha kuwa mchezaji huyo amefariki leo nyumabani kwake Rome japokuwa hakusema tatizo gani lilimuondoa mzee huyo wa miaka 87 ambaye aliwahi kuweka takwimu ya mwaka wakati huo alipotoka , Sweden na kujiunga na Charlton Athletic mwaka 1951, alijiunga na Napoli akitokea Atalanta kwa pesa za kitaliano ITL 150m 1952.
Jeppson alifunga mabao 52 katika mechi 112 alizochezea Napoli na amekuwa mchezaji anayekamata nafasi ya kumi na moja katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo mchezaji huyo alipata umaarfu mkubwa sana kusini mwa italia na tumeomba kumpa heshima katika mechi yetu dhidi ya Udinese katika ligi ya Serie A siku ya jumatau usiku.
,Rais wa timu hiyo Aurelio De Laurentiis ameelezea hisia zake kuhusu kifo cha mchezaji huyo Hans Jeppson, kuwa ni moja kati ya wachezaji bora kupata kutokea katika historia ya klabu hiyo na tutakaa kimya kwa dakika moja kumshukuru mchezaji huyo ."
Jeppson aliichezea mara 12 Sweden, na kufunga magoli Tisa na kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1950 Nchini Brazil™
No comments:
Post a Comment