Mchezaji wa zamani wa  Bolton Wanderers  Fabrice Muamba ndiye atakaye kuwa mgeni rasmi na kukabidhi kikombe kwa mshindi wa kombe la CAPITAL one siku ya jumapili kati ya  Bradford City na Swansea City katika uwanja wa  Wembley.
Akiwa kama mgeni rasmi atafanya majukumu yote anayofanya mgeni rasmi wakati wa mechi na atatazama mechi hiyo katika chumba cha kifalme  Royal Box.  Muamba  24-alilazimika kustaafu soka baada ya kupata tatizo la ugonjwa wa mshtuko wa moyo  katika mechi dhidi  Tottenham Hotspur kwenye kombe la FA moyo wake ulisimama  kufanya kazi kwa dakika  78
"Yamekuwa mashindano mazuri sana kwangu na  hii ni heshima kubwa kupewa nafasi ya mimi kuwa mgeni wa heshima katika mechi hiyo ," Muamba . "Najua itakuwa wakati mzuri sana jumapili ."