TAARIFA KWA UMMA
FEBRUARY 6, 2013
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight)
Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana
walio chini ya miaka 25 uzito wa Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la
ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday
Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.
IBF imeamua kumpatia
Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia kwa vijana baada ya kuangalia
mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza
kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia wengi wa
Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa nyingi
walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo kuweza kupanda chati kwenye
viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na
Oscar De la Hoya.
Kama Shauri atashinda na
kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa
duniani kama kina Dong King, Bob Arum na wengine wengi. Nafasi kama hii inaipa
nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya kujitangaza kibiashara na utalii kwani
dunia inaiona kuwa kati ya nchi zinazotoa mabingwa wa dunia.
Kama Shauri atashinda
taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu historia ya ngumi nchini kuweza
kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya manne duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO
na WBA.
Shiriksiho la Ngumi la
Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina makao yake makuu ya kuhudumia bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ndilo lililomtafutia Shauri nafasi
aliyopata.
IBF/Africa inawahamasisha
Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao pamoja na makampuni mbalimbali
bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia Shauri ufadhili wa kuweza
kuligombea taji hili.
Mungu mbariki bondia
Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amen.
Imetolewa na:
UTAWALA
Shiriklisho la Ngumi la
Kimataifa Afrika (IBF/Africa)
Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment