Kampuni ya Nike ilifutilia mbali
tangazo hilo la biashara huku athari za kutumia wanariadha kutangaza
bidhaa za makampuni zikipigwa darubini kwa mara nyingine.
"Mimi ndio risasi katika chemba" ndiyo maandishi ya
tangazo la kibiashara la kamapuni ya bidhaa za michezo ya Nike
ikimuonyesha bingwa wa michezo ya Olimpiki Oscar Pistorius.
Huku mwanamichezo huyo akikabiliwa na kesi ya
mauaji ya mchumba wake Reeva Steenkamp, ambayo viongozi wa mashtaka
wanasema ni ya kupangwa, wahisani wake walilazimika kufanya mikutano ya
dharura.
Pistorius, ambaye amekanusha vikali mauaji hayo,
anasemekana kujipatia mamilioni katika matangazo ya biashara ya
makampuni ya Nike, BT, Thierry Mugler, Oakley na Ossur,kampuni moja
nchini Icelandi ambayo hutengeza miguu ya vyuma aliyokuwa anatumia
mwanariadaha huyo.
Bidhaa mbaya
Lakini kama ilivyodunia rangi rangile kwenye
michezo, mkimbiaji wa vyuma kama anavyojulikana, huenda akapoteza kila
ya matangazo hayo ambayo yalikuwa yanamletea mamilioni ya pauni hata
ikiwa hatapatikana na hatia.
Ilipoulizwa ikiwa inatafakai kuondoa matangazo ,
ya Pistorius, ambayo yanaaminika kuwa na thamani ya dola milioni mbili,
msemaji wa kampuni hiyo alisema bado wanatazama hali itakavyokuwa kwani
ni jambo linalohusisha polisi.
Mhisani mwingine wa Pistorius, M-Net Movies, ambayo ni runinga ya
kulipia Afrika Kusini , ililazimika kuodoa matangzo yake ya kibisahara
ambayo Oscar alihusika nayo.
Kupitia kwa Twitter, M-Net ilitoa rambi rambi
zake kwa familia ya marehemu na kasha ikasema kuwa haina budi ila
kuondoa matangazo yake ya Oscar kwenye televisheni yake mara moja.
John Taylor, mkurugenzi wa kampuni inayotumia
wanamichezo katika matangazo yao ya kibiashara, aliambia BBC kuwa "hata
kama pistorius hatapatikana na hatia, sifa yake imeharibika. Kamapuni
yanapaswa kuchukua hatua za haraka kujitenga naye , hayawezi kusubiri
hadi kesi itakaposikilizwa."
Mchumba wa Pistorius
"Sio kama panya kutoroka meli inayozama, kwa swala hili inaonekana ni
hatua muhimu itakayochukuliwa, alisema msemaji huyo," alisema Taylor.
Naye Nigel Currie, mkurugenzi wa kampuni ya
matangazo ya biashara katika michezo, Brand Rapport, anakubaliana na
hilo akisema kuwa hili ni tofauti kabisa ikilinganishwa na yale
aliyokumbwa nayo Tiger Woods na Lance Armstrong, kesi hii inahusu maisha
ya mtu. Hakuna atakavyoweza kutokamana na jambo hili.
Lakini hakuna hata mhisani wake mmoja amevunja uhusiano naye na nyingi ya kampuni hizo zimekimya hata sasa.
Kampuni ya mitindo Thierry Mugler,iliyomteua
Pistorius kuwa sura ya mafuta yake ya wanaume, mwaka 2011, ilisema kuwa
hawana tamko lolote kuhusiana na kashfa hii na kusema uamuzi hauwezi
kuchukuliwa kwa sasa.
Kampuni ya Nike huwatumia wanamichezo wanaoweza kuziweka bidhaa zake katika hadhi ya juu kabisa
Pistorius alikuwa na sifa ya kung'ang'ana ili
kushinda , ari ya ushindi aliweza kufanikiwa licha ya kuwa mlemavu hali
iliyomfanya kuwa mchezaji mzuri wa kutumiwa kutangaza bidhaa za makapuni
ya vitu vya michezo.
Lakini kufuatia tukio la wiki jana, makampuni
mengi sasa huenda yakatafakari mara mbili ikiwa yataendelea kumtumia
Oscar kutangza bidhaa zao. Na sasa pia huenda wakawa makini sana na
wachezaji wanaowatumia.
Katika hii dunia ya pesa na michezo, huenda akajipata ametupiliwa mbali ikiwa ana hatia au la.
No comments:
Post a Comment