Nigeria imeifunga mali magoli 4-1, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika.
Elderson Echiejile amefunga magoli mawili katika dakika ya 25 na 30.
Goli la tatu limefungwa na Emenike katika dakika ya 44 baada ya mpira aliopiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.
Kipindi cha kwanza kimemalizika na sasa ni mapumziko, Nigeria ikiongoza kwa magoli 3-0.
Ahmed Musa amezidi kufifisha matumaini ya Mali kucheza fainali baada ya kupachika goli la nne dakika ya 60.
Mali haikuonyesha kukata taama japo muda japo muda ulizidi kuyoyoma, kwani katika dakika ya 70 Cheikh Diarra aliifungia bao timu yake.
Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast, timu ambayo
ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa
wachezaji wake.
Katika mchezo na Ivory Coast, Nigeria walishinda magali 2-1.
Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika
Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza
dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.
Timu nyingine katika nusu fainali za Afcon ni
Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika
hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo
kwa goli 1-0.
No comments:
Post a Comment