Haruna Niyonzima akiongea na Ladislau Mbogo asubuhi ya leo walipokwenda wachezaji wa Yanga kumjulia hali hospitali |
Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Ladislaus Mbogo anaendelea
vizuri baada ya jana kufanyiwa upasuaji wa uvimbe (shavuni) katika
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam, upasuaji uliofanyika
chini ya usimamizi wa daktari wa timu ya Young Africans Dr Nassoro
Matuzya.
Mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini
Kijitonyama, wachezaji wote wa Young Africans pamoja na benchi la ufundi
waliongozana kwenda Hopsitali ya Mwananyamala kumpa pole Mbogo ambaye
jana alifanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu ya shavu la kushoto.
Akiongea
leo asubuhi baada ya kutembelewa na wachezaji na benchi la Ufundi,
Mbogo amesema anajisikia vizuri, anamshukuru mungu upasauji umeenda
vizuri na hali yake inaendelea kuimarika hivyo anaamini muda si mrefu
atarudi katika hali yake ya kawaida.
Mbogo
ambaye alisajiliwa mwaka jana katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom
2012.2013 akitokea timu ya Toto Africans, amekifikia hatua hiyo ya
kukubali kufanyiwa upasuaji kufuatia kufanyiwa uchuguzi na madakatari
kutoka hospital ya Mwananyamala.
Dr Nassoro Matuzya
akiongea kwa niaba ya madaktari waliomfanyia upasauaji, amesema upasuaji
ulifanikiwa kufanyika salama kabisa, tulimfanyia upasuaji jana asubuhi
kufikia mida ya mchana tayari tulikua tumeshamaliza na kwa sasa yupo
wodini kwa mapumziko chini ya uangalizi wa madakatari.
Kwa mujibu
wa daktari wa Yanga, Dr Matuzya, Mbogo atakua nje ya uwanja kwa kipindi
kisichopungua wiki tatu akiendelea kuunguza sehemu aliyofanyiwa
upasuaji.
Katika hatua nyingine Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi yake katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Ruvu Shooting, mchezo utakaofanyika siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha wachezaji 25 kipo kambini katika hosteli za klabu zilizopo mitaa ya Twiga/Jangwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi, mchezaji pekee ambaye hayupo kambini ni Ladislasu Mbogo ambaye amedanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu ya shavuni.

No comments:
Post a Comment