Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia
kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.
Mechi
hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia
zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya
Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha
wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini
Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa
Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga),
Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo
ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba),
Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas
Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali
ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh
(Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso
(Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda
(Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
No comments:
Post a Comment