HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 March 2013

MACHAFUKO YA KISIASA YACHELEWESHA FEDHA ZA SIMBA

http://www.tunisienumerique.com/wp-content/uploads/ess_grand.jpg
Klabu ya Etoile du Sahel inayoshiriki Ligi Kuu ya Tunisia imeandika barua kwa uongozi wa klabu ya Simba ukiomba msamaha kwa kuchelewa kulipa dola za Marekani 300,000 (Sh. 480) ambazo ni kwa ajili ya malipo ya mchezaji Emmanuel Okwi aliyeuzwa na 'Wanamsimbazi' kwenda kwa vigogo hao wa Tunisia kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Barua ya Etoile iliyosainiwa juzi (Machi 13) na katibu mkuu wa klabu hiyo, Adel Ghith , ilisema kuwa wamechelewa kukamilisha taratibu za malipo hayo kutokana na kusubiri kibali maalumu ambacho hutolewa na benki kuu ya nchi yao.

Ghith aliendelea kueleza katika barua yake hiyo aliyoielekeza kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, kuwa matatizo ya kiuchumi yaliyojitokeza nchini kwao kufuatia machafuko makubwa ya kisiasa ndiyo yamechelewesha dhamira yao ya kutaka kuimiza makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili hizo wakati wakikamilisha mauzo ya Okwi, lakini akaahidi kuwa ni lazima walipe deni hilo na Simab waendelee kuwa na subira.

"Etoile du Sahel ni klabu kubwa na kwa kila msimu huwa na wachezaji wa kigeni wasiopungua watatu katika kipindi cha miaka 20, tunaahidi tutatimiza makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili hizi," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema  kuwa nao waliwajibu Etoile du Sahel kwamba wamechoka na hali ya kucheleweshewa malipo hayo, hasa baada ya kuona kuwa wamekaa kimya kwa muda mrefu.

Mtawala alisema katika barua yao ya , wamewataka Etoile sasa wawalipe fedha hizo kwa mkupuo na siyo  kwa awamu tena kama walivyokubaliana awali.

Aliongeza kuwa vilevile, wamewataka Etoile waseme wazi ni lini watawalipa fedha zao na kwamba, endapo watashindwa kufanya hivyo, ndani ya wiki moja Simba itachukua hatua zaidi za kutafuta haki yake.

Wakati Simba wakiendelea kuzungushwa juu ya malipo ya fedha zao, Okwi ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda alisharipoti kitambo katika klabu yake hiyo mpya nchini Tunisia na kuanza kuitumikia.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers