Chama cha mchezo wa Tenis Tanzania (TSA) kinatarajia kuandaa michuano ya kuogelea kwa Nchi za Afrika mashariki yatakayo fanyika jijini Dar es Salaam.
ambapo Tarehe ya mashindano itatangazwa hapo badae ,Mkurugenzi wa ufundi , Marcelino Ngalioma amethibitisha .
Amesema kuwa TSA imeshatuma baraua za mialiko kwa Malawi, Kenya,
Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, (DRC) na
Mozambique.
Ngalioma ameongeza kwa kusema TSA bado ipo katika majadiliano na wadhamini ili waweze kujua hata sehemu ambayo mashindano hayo yatafanyika .
Mkurugenzi huyo wa ufundi amesema kuwa TSA inatumai kuwa mashindano hayo yataongeza ubora wa viwango kwa wachezaji wake .
“Mashindano hayo ni moja kati ya michuano mikubwa zaidi na inahitaji msaada mkubwa ili kuweza kufanikishwa na tunayaomba makampuni kutuunga mkono ili kufanikisha mashindano hayo
Aidha maesema ukiacha la kuwaomba wadhamini ameongeza kwa kusema watafanya mashindano kwa kuzingatia viwango vya olimpick kwa kuweka mabwawa ya mita 50 na 100 ili kuweza kukidhi viwango vya Olimpik
Ngalioma amethibitsiha kuwa zaidi ya washiriki 260 wamekwisha kujiandikisha katika mashindano yatakayofanyika kuanzia kesho katika shule ya Heaven Of Peace Academy (HOPAC) iliyopo maeneo ya Mbuyuni kunduchi jijini Dar es
Salaam.
mashindano hayo ya kesho watayatumia kutazama takwimu za taifa za kuogelea
“Tuna waogeleaji wengi kutoka Mwanza,
Shinyanga, Zanzibar, Morogoro, Arusha na Dar es Salaam. na wengine ni wa Tanzanian ambao wanaishi Kenya,” aliongeza .
Katika mashindano hayo ya mwishoni mwa juma waogeleaji 20 wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Shirikisho la africa kuogelea (CANA) katika mashindano ya Zone 3 & 4 yatakayo fanyika
Lusaka mwezi ujao .
“kwa mwaka jana tulishiriki mashindano hayo na tulishinda Nishani nne fedha moja na tatu na shaba
TSA itaandaa mashindano ya taifa mwezi kenda tarehe 7 - 8 jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment