Phil Jones atakuwa nje katika mechi ya Manchester's United' itakapo pambana na Real Madrid katika mechi ya mkondo wa pili ya Ligi ya mabingwa Barani Ulaya baada ya kuumia kifundo cha mguu .
ilikuwa ikifikiriwa kuwa kijana huyo mwenye miaka
21- angejumuika na wenzake kwenye mazoezi leo asubuhi lakini hakuwepo .
na Feg amethibithisha kuwa hatocheza mechi hiyo
mchezaji huyo alikuwa moja kati ya wachezaji walionyesha uwezo mkubwa katika mechi ya mkondo wa kwanza kule Bernabeau, .
Ferguson : "Ni Tatizo, lakini jambo ambalo limekuwa nje ya uwezo wetu lakini tunawachezaji mmbadala nina imani nitapata mchezaji sahihi ."
Mchezaji huyo aliumia wakati wa mechi ya FA CUP dhidi ya
Reading .
Robin van Persie, Patrice Evra na Danny Welbeck wamerejea katika hari yao ya kawaida katika ushindi wa 4-0 Dhidi ya Norwich siku ya Jumamosi ,
wote walifanya mazoezi leo Asubuhi.
Madrid ikichagizwa na ushindi mara mbili mfululizo dhidi ya wapinzani wao wakubwa Barcelona watakuwa wanachagizwa na urejeo wa Nahodha wao Nahodha Iker Casillas,
ambaye ni moja kati wachezaji 24 walio wasili leo jijini Manchester .
Mchezaji huyo ni mshindi wa kombe la dunia amekuwa nje ya kiwanja mara kdhaa tangu Mwezi January Real Madrid inakwenda na mchezaji Gumzo wa klabu hiyo ambaye aliwahi kuchezea Manchester united Miaka ya Nyuma Cristiano Ronaldo na itakuwa anarejea kwa mara ya kwanza katika uwanja huo tangu alipouzwa miaka sita iliyopita .
Mechi ya kwanza Timu hizo zilitoka sare ya goli moja kwa moja Ushindi wa aina yoyote utazifaa Timu zote mbili suluhu ya zaidi goli moja itaifaa real madrid au suluhu ya kuto kufungana utaifaa United .
No comments:
Post a Comment