HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

20 March 2013

MIL 30 ZAUWEKA REHANI UCHAGUZI WA CHANETA WASOGEZWA MBELE MWEZI MZIMA


Uchaguzi wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) uliotarajiwa kufanyika mkoani Dodoma Jumamosi ijayo (Machi 23) sasa umesogezwa mbele hadi Aprili 20.

 Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Michezo Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), John Chalukulu, amesema kuwa sababu ya kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo ni kukosekana kwa fedha za maandalizi.

 Chalukulu amesema kuwa ili kuendesha uchaguzi huo, kiasi cha Sh. milioni 30 kinahitajika lakini ameahidi kuwa BMT, kwa kushirikiana na Chaneta, watahakikisha fedha hizo zinapatikana kabla ya siku mpya iliyopangwa kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

 Amesema kuwa baada ya mabadiliko hayo, sasa zoezi la usaili kwa wagombea litafanyika Dodoma Aprili 18 na siku inayofuata itakuwa ni ya kujadili pingamizi endapo zitakuwapo na kwamba, wagombea wote watakaopitishwa kuwania nafasi mbalimbali zilizopangwa watajulikana siku hiyo hiyo.

 "Tunawaomba radhi wadau wote wa Chaneta ambao walikuwa wamejiandaa kuelekea mkoani Dodoma kwani uchaguzi huo umesogezwa mbele... lakini taratibu nyingine zilizokuwa zimefanyika awali ikiwamo ya utoaji wa fomu zinabaki kama zilivyo," .
Katika uchaguzi huo, nafasi inayoonekana kuwa na upinzani mkali ni ya mwenyekiti ambapo aliyekuwa katibu mkuu, Anna Kibira, anatarajiwa kuchuana na makamu mwenyekiti, Shy-Rose Bhanji.

Anna Bayi ambaye alikiongoza chama hicho ameamua kutogombea tena safari hii pamoja na katibu msaidizi wake, Rose Mkisi, ambaye alikaimu nafasi ya Kibira aliyekuwa amesimamishwa na chama hicho kwa muda mrefu.

Kutokana na mabadiliko ya katiba ya Chaneta, sasa katibu mkuu atakuwa ni wa kuajiriwa na hivyo mchakato wa kumpata utatekelezwa kwa kufuata taratibu za ajira baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu huo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers