Aliyekuwa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Finny Muyeshi, aliyefariki dunia Jumatano iliyopita anatarajiwa kuzikwa Jumamosi katika mji wa Busia ulioko Magharibi ya Kenya, imeelezwa jana.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, amesema kuwa maandalizi ya mazishi ya afisa huyo ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti la East African Standard yako katika hatua za mwisho kwa kushirikiana na familia yake.
Musonye amesema kwamba kuondokewa kwa afisa huyo ni pigo katika shirikisho hilo na kamwe hawatasahau mchango wake katika maendeleo ya soka ya ukanda huo.
"Mazishi yatakuwa Jumamosi nyumbani kwao Busia... tunakamilisha taratibu za mwisho," Musonye.
Marehemu Muyeshi alifariki dunia Machi 13 mwaka huu katika hospitali ya Coptic iliyoko jijini Nairobi ambako alikuwa akipatiwa matibabu kufuatia maradhi ya figo yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
Marehemu Muyeshi ambaye ni Mkenya ameitumikia CECAFA tangu mwaka 2002 akiwa ni msaidizi wa Musonye katika kusimamia mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) pamoja na michuano ya Kombe la Chalenji ambayo hufanyika kila mwaka katika ukanda huu.
Kutokana na kusumbuliwa na maradhi hayo, hakuweza kuitumikia CECAFA tangu mwaka juzi.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi,.

No comments:
Post a Comment