Habari Leo wasomaji wangu wa
K-sport.com leo nimeona tuzungumzie uendeshwaji wa vilabu viwili vikongwe hapa
nchini simba na yanga mbavyo Huwa haviishi migogoro kila kukicha ,jambo kuu
moja la kutazama leo hii ni kutaka kuangilia nini cha kufanya ili klabu hizi
mbili ziondokane na migogoro isiyokwisha kila siku .
Moja kati ya jambo kubwa na la msingi
ni kubadili aina ya uendeshaji wa vilabu hivi ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa
vikitumia mfumo wa wanachama katika kuendesha klabu hizi lakini jambo moja la
msingi ambalo nataka kuwaeleza mashabiki na viongozi wa vilabu kama wataendelea
na utaratibu wa sasa kamwe hawataendelea mpaka nabii isah (Yesu) atakaporejea tena
kuhumu vilabu ambavyo vimepoteza muda wao wa kuishi dunia pasipo kufanya
maendeleo ya kimsingi .
Je ni mfumo gani ambao vilabu hivi
vinahitaji kutumia kiundeshaji vilabu lazima kutumia mfumo wa hisa kama baadhi
ya vilabu au makampuni makubwa yanavyofanya sehemu mbalimbali duniani ikwemo
bara la afrika Yanga na Simba zinawachama wengi ambao hata kama mfumo
ukibadilishwa wataweza kuhimili kwa kugawanya kwa makundi tofauti ya
bei za hisa kwa mfano kuweka viwango vya hisa kuanzia , milioni moja, laki moja, Elfu hamsini ,Elfu thelathini ,Elfu ishilini elfu kumi na ,Elfu tano
kuwa kiwango cha mwisho na kila kiwango kiwe
na asilimia ya uwakilishi katika bodi na kwa muda mfupi unaweza kupata mamiliano
ya shilingi na kupata ya kuwalipa kwanza waaanzilishi wa vilabu .
Kwa utaratibu simba na yanga itakuwa
na uwezo wa kwenda kukopa Benki na kujenga kiwanja na maduka ya kisasa ambapo
wanachama wenye hisa zao watakuwa Mdhamana wa klabu hiyo kwa kiasi kikubwa cha
pesa walichopata kwa utaratibu wa hisa na itakuwa rahisi kudhaminika katika
mabenki na kupata fedha za kujenga viwanja na maboresho kadhaa kwa pesa za
wanahisa klabu itapata fedha za kulipa wachezaji wake wahudumu wa kila siku wa
klabu na mahitaji ya klabu kwa ujumla na kuanza kusimamisha vyanzo sahihi vya
uuzaji bidhaa zinazohusiana na nembo ya timu husika kuweka viwango vya ununuaji
hisa kwa kutazama viwango vya pesa hii itakuwa jambo la msingi kwa kila mtu
kutokana na hari yake ya kiuwezo .
Ukitazama mfano wa klabu ndogo ya
Azam ambayo inaleta mapinduzi ambayo kwa sasa inamilikiwa na kampuni ya
uzalishaji vyakula ya Bakhresa ni wazi uongozi wa klabu wanaufahamu kuwa
unakwenda mbali zaidi kutazama nini mahitajitaji ya klabu kwa sasa jambo kuu ni
kuwa uongozi wa vilabu hiki unaelewa nini klabu inataka tofauti na Simba na
yanga ambavyo bila kulumbana havisikiii raha hatakidogo .
Na wapo baaadhi ya viongozi kwenye
vilabu ambayo hawajui hata sheria za soka achana na kuuchezaa mpira wenyewe
sheria za hawazijui labda kucheza Criket ndiko wanakoweza viongozi wengine
huleta siasa mpirani kugombana na wanachama kila kukicha klabu inayogombana na
wanachama kila kukicha haiwezi kufikiria maendeleo ya soka kama ujenzi wa
viwanja na maendeleo ya klabu viongozi wa vilabu hivi hufukiria kununua
wachezaji kwa pesa nyingi na wachezaji wenyewe wakati mwingine hawana hata
viwango vya kimataifa vya kucheza soka kabisa .
Ili simba na yanga zifanikiwe hazina
budi kufuata mfumo mpya wa soka wa uendeshaji kimataifa ambao unatumika hasa
katika Nyanja za kimataifa kwani kwa mfumo ambao wanatumia sasa unawapa nafasi
baadhi ya matajiri ambao lengo lao ni kutaka kukwepa kodi kufanya biashara
haramu na kutaka kuiibia serikali katika mapato na kutaka kujenga vitu ambavyo
hazina msaaada kwa klabu na kujinufaisha watu binafsi ni aibu kuona klabu kama simba au yanga haina uwanja wake binafsi hii ni aibu tena fedheha ya aina yake
ningekuwa mimi ndio kiongozi wa klabu kama hii nisingegombea uongozi wa klabu
kama hii kwani ni aibu kubwa na fedheha isiyopimika .
Ni sawasawa na kujenga shule ambayo haina wanafunzi walimu
wala vitabu.
No comments:
Post a Comment