Mohammed Banka anayecheza Kenya amelitaka Shirikisho la Soka (TFF) kufuatilia kwa nguvu zaidi Watanzania walio nje ya nchi ili wapate fursa ya kuitwa kwenye timu ya taifa.
Ni washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu pekee wa TP Mazembe ya JK Kongo ambao wameitwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachocheza na Morocco katika pambano la michuano ya awali ya Kombe la Dunia kesho.
Kiungo huyo anayeichezea timu ya ligi kuu ya Kenya ya Bandari ya Mombasa, amesema nje ya nchi wapo wachezaji wanaofanya vyema lakini hawapati nafasi ya kuitwa timu ya taifa kwa vile hawafuatiliwi kwa ukaribu na shirikisho.
"Nadhani kuna haja TFF ijenge utamaduni wa kuwafutilia wachezaji wa nje ya nchi kwa vile wapo wanaoweza kuwa msaada wa timu za taifa, lakini hawapati nafasi hiyo," alisema.
Alisema kusiwe na utamaduni wa kuwafuatilia wachezaji fulani tu na kuwapa nafasi bali waangalie wachezaji wote wa nje ambao ni hazina na faida ya nchi kama wakitumiwa kulingana na uwezo wao.
"Kama mataifa mengine yanavyofuatilia wachezaji wao na kuwatumia katika timu zao za taifa, nasi tunapaswa tufanye hivyo," alisema.
"Wapo wachezaji wanafanya vizuri lakini hawaitwi timu ya taifa kwa vile hawafuatiliwi.
CHANZO NIPASHE

No comments:
Post a Comment