Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi zawadi kwa Nahodha wa timu
ya makonde Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa
mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)
kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto
pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke
Naibu
waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima akikabidhi mfano wa hundi
ya shilingi millioni moja kwa Nahodha wa timu ya Mbezi Ally Shila
Kulola baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya
mpinga Cup kwa kushinda Makondeko mabao 7-6 katika mikwaju ya Pernaty
Timu
ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda
ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa
michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay
police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 baada ya kupiagiana mikwaju ya penati na kuibuka washindi
Michuano ya mpinga Cup imemalizika
rasmi jana baada ya mchezo wa fainali katu ya timu ya Mbezi na
makondeko ambapo, timu hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye
mkwaju wa penalti ambapo timu ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6
.
Katika michuano hiyo iliyodumu kwa
muda wa juma moja na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa
kipolisi wa kinondoni timu ya mikocheni Iliibuka kuwa mshindi wa tatu
wa michuano hiyo.
Akiongea wakati wa kufunga michuano
hiyo mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima
alisema” anawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini ambao ni
Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa
ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano
haya yanafanyika kwa mafanikio.
Hii nijitahada ya pekee kuunganisha
michezo na elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa
tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha pikipiki kwa
muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato
kwa michezo ni ajira.
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama
barabarani SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano
hii na kusisitiza wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila
shurutishi.
Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa
Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya
mvuto mkubwa kwa washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi
mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha
watumiaji wa barabara waliokuwa wakihudhuria hapa.
Tunaamini kuendelea na juhudi hizi
tutaweza kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea
kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika shughuli
mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani
Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya
kinondoni imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia
katika mkoa wa ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii
nchini nzima.
No comments:
Post a Comment