MCHEZA soka nyota wa
Brazil, Bruno Fernandes amehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na kosa la
kuamuru mauaji ya rafiki yake wa kike wa zamani. Nyota huyo pia alikutwa na hatia ya kuuficha mwili wa Eliza Samudio na kumteka mtoto wao wa kiume mwaka 2010.
Fernandes
ambaye ni golikipa wa zamani wa klabu ya Flamengo alikiri kufahamu kuwa
Samudio alinyongwa na mwili wake kupewa mbwa wale lakini alikataa kutoa
amri ya kumuua mwanamke huyo.
Mauaji hayo yalivutia vyombo vingi vya habari vya Brazil ambapo yalikuwa yakifananishwa na kesi ya OJ Simpson huko Marekani. Fernandes
ambaye alikuwa maarufu kwa mashabiki wa soka wan chi hiyo alikuwa
akipigiwa chepuo kucheza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
Mmoja
wa marafiki zake, Luiz Henrique Ferreira Ramao na polisi wa zamani
Marcos Aparecido dos Santos nao pia walihukumiwa kutokana na mauaji ya
Samudio.
No comments:
Post a Comment