Timu ya soka ya Azam fc imesonga mbele katika hatua inayofuata ya kombe la shirikisho baada ya kwenda suluhu na Barack young controlers ya liberia kwenye mchezo uliofanyikaa katika uwanja wa a taifa jijini Dar es salaam timu ya azam ilikosa nafasi mbili za wazi hasa kipre tcheche ambaye alibaki yeye na mlinda mlango na kukosa goli la wazi licha ya ndugu yake kumuomba pasi akiwa pembeni .
Azam inasonga mbele kwa mabao mawili kwa moja ambayo walipata katika mechi ya kwanza iliyofanyika nchini Liberia sasa azam itacheza na Rabat ya Moroco majuma mawili yajayo .
No comments:
Post a Comment