Zaidi
ya mawakala 15 tayari wamewasiliana na Kampuni ya Tanzania Mwandi kuwahitaji
wachezaji mbalimbali kwaajili ya kuwapeleka kwenye klabu za barani Ulaya, Asia
na Afrika ili kucheza soka la kulipwa.
Mwitikio
huo umeongezeka kutokana na vijana wa kiafrika kuwa na soko kubwa katika
ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu kwa nchi mbalimbali kama Sweden, Uholanzi,
Denmark, Ureno na nchi nyinginezo.
Arne
Anderson kutoka AA Football Service ya Sweden amesema kuwa binafsi yuko tayari
kuchukua wachezaji wawili kwaajili ya kuwatafutia clubs nchini humo kwani
tayari mafanikio ya wachezaji watano wa kiafrika aliowapeleka yamempa maombi ya
timu nyingi za Sweden.
“Niko
tayari kuchukua wachezaji wawili endapo tutakubaliana kuhusu maslahi yangu
pindi wachezaji hao wakianza kucheza hapa”, Arne amesema.
Kutokana
na mafanikio hayo na maombi ya mawakala lukuki Kampuni ya Tanzania Mwandi
inazidi kuwasisitizia wachezaji wa Kitanzania kujaza fomu zinazopatikana
kupitia blog.tanzaniamwandi.co.tz ili
kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Sweden, Norway, Denmark, Uholanzi,
Ureno, Uswiss, Ufaransa na Ubelgiji, barani Asia (Kuwait, China, Qatar nk) na
klabu nyingine barani Afrika.
Mpaka
sasa jumla ya wachezaji wa kitanzania 15 wamekwishajaza fomu za haraka kwenye
tovuti ya Tanzania Mwandi huku kampuni ikiwa imepokea pia maombi ya wachezaji
25 kutoka nje ya nchi.
“Maombi
yanazidi kuja ingawa tunawahimiza Watanzania wasikimbie kiingilio cha shilingi
300, 000 wakumbuke kuwa wanafanya majaribio wakiwa nyumbani na watakapopata
timu Kampuni ya Tanzania Mwandi haitachukua chochote kwenye mikataba yao, ni
wao na mawakala ndio watakokubaliana juu ya watakachokipata kutoka kwa klabu
husika”, alisema Teonas Aswile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, waandaaji
wa African Youth Football Tournament.
Aswile
amezialika klabu mbalimbali za ligi kuu ya soka Tanzania Bara na Visiwani
kutazama wachezaji watakaofika katika michuano hiyo kwani wapo baadhi ya
wachezaji kutoka nje ya nchi ambao watafika na wangependa kucheza soka la
Tanzania.
“Kati
ya wachezaji 25 wa nje ya nchi wengine wameomba tuwatafutie timu hapa nchini
hivyo klabu zikija zinaweza kuwapata wachezaji hao wakiwa huru kwasababu
watakuja kwa gharama zao kufanya majaribio nchini. Pia klabu hizo zitumie fursa
hii kuuza wachezaji wake.”
Michuano ya African Youth
Football Tournament inatarajia kufanyika Juni 10 hadi 14 mwaka huu katika
uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kati ya miaka 18
hadi 21 kutoka Tanzania na bara zima la Afrika
No comments:
Post a Comment