Baada ya kujipima na timu 'vigogo' barani Afrika za Zambia na Cameroon
kabla ya kuwanyuka 3-1 mabingwa wa zamani wa Afrika, Morocco, timu ya
taifa ya Tanzania inatarajia kupiga kambini nchini Algeria kujiandaa kwa
mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika
Brazil mwakani.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, kocha wa Taifa Stairs, Kim Poulsen ambaye alikuwa akishuhudia mazoezi hayo, alisema kuwa timu yake itaweka kambi Algeria mwezi ujao na kwamba wakiwa huko, watacheza mechi kadhaa za kirafiki dhidi ya timu zilizowazidi viwango, wakiwamo wenyeji wao Algeria ambao hivi sasa wanashika nafasi ya 35 kwenye viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na Fifa wiki iliyopita.
Licha ya kupanda kwa nafasi tatu, Tanzania bado iko chini kwenye viwango hivyo kwani sasa inakamata nafasi ya 116.
"Nimependekeza timu iweke kambi Algeria kabla ya kutua Marakech kucheza na Morocco. Mazingira ya Algeria yanafanana na ya Morocco, hivyo ni vyema timu ikae Algeria kwa muda mrefu ili kuzoea hali ya hewa ya huko," alisema Poulsen.
"Tukiwa huko tutacheza mechi za kirafiki dhidi ya Algeria na timu nyingine kubwa ambazo nimewaambia viongozi wa TFF watutafutie," aliongeza Poulsen, bila kuzitaja timu hizo.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alikiri jana kuwa wamepokea mapendekezo ya benchi la ufundi la Stars linaloongozwa na Poulsen, lakini akiahidi kutoa ufafanuzi zaidi baadaye, akisema: "kuna siku maalum ya kulizungumzia hilo."
Kabla ya kucheza dhidi ya Morocco, Stars ilijipima dhidi ya Zambia na kushinda kwa bao 1-0, kisha ikapata ushindi mwingine kama huo dhidi ya Cameroon. Mechi zote hizo zilichezwa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
MKATABA MPYA
Katika hatua nyingine, kocha Poulsen alisema kuwa hana wasiwasi na hatma yake Stars baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kumalizika Machi 15 kwani anaamini kuwa vijana wake wako katika mwelekeo mzuri.
Poulsen aliongeza kuwa hadi sasa, tayari mwajiri wake (TFF kwa kushirikiana na serikali) amemhahakikishia kumpa mkataba mwingine utakaokuwa mrefu zaidi na kwamba watausaini wakati wowote watakapokamilisha baadhi ya mambo.
TFF kupitia katibu wake, Osiah ilishakubali kumuongezea mkataba Poulsen na sasa inasubiri ruhusa ya serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ndiyo humlipa mshahara kocha huyo.

No comments:
Post a Comment