Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka
nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya
upembuzi yakinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda
stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa
Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema
upembuzi yakinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa
mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na
michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya
Yanga.
Zhang alisema kwamba
kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali
duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es
salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya
kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city)
uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.
Aidha
Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium
(jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi
Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa
kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba
watazamaji 20,000.
Katika uwasilishaji huo wa makadirio
ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya
Yanga Francis Kifukwe alisema wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa
kukamilisha zoezi la upembuzi yakinfu mapema ambapo leo wamepata fursa
ya kujionea na kujua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
Kufukwe
alisema wamepewa nafasi ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa
klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha
kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mktaba
kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda.
Akijibu swali
la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za
ujenzi wa uwanja, Kifukwe alisema ujenzi wa uwanja wa mpya utajengwa na
wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga.
Kwa
mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa
uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia
utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013
kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.
Kaunda
stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye
viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu
maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari,
eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja
vya michezo.
No comments:
Post a Comment