Shirikisho la soka la Cameruni limemteua Volker Finke kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imetangaza majira ya saa mbili usiku katika kipindi cha newscast.
Mzee huyo mwenye miaka 65-raia wa ujerumani atakiongoza kikosi hicho hadi mwaka ujao huku akitarajiwa kuongoza timu hiyo kwa miaka minne zaidi . ofa ya kutafuta kocha wa cameruni ilitangzwa mwezi April 22 ambapo maafisa wa shirikisho la soka cameruni walitoa majina ya watu walio omba kazi hiyo huku makocha nguli kama Domenech, Eriksson, Lechantre na Finke ambaye ndiye aliyepata kazi akiwemo na anachukua nafasi ya Jean Paul Akono raia wa cameruni ambaye aliamua kutokuomba kazi hiyo ,
kocha huyo anavibarua vigumu katika timu hiyo ikiwemo kuifunga timu za Ukraine, Togo na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa kongo . lakini watu wengi wanaamini kuwa mkufunzi huyo ataanza kazi hiyo mapema zaidi kutokana na hari ya kiafya ya kocha huyo wa sasa japokuwa shirikisho halijatangaza hasa ni lini mkufunzi ataanza kazi rasmi ya kuionoa timu hiyo .
No comments:
Post a Comment